GET /api/v0.1/hansard/entries/561839/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 561839,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/561839/?format=api",
    "text_counter": 83,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Kombe",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 250,
        "legal_name": "Harrison Garama Kombe",
        "slug": "harrison-kombe"
    },
    "content": "Asante, mhe. Naibu Spika, kwa kunipatia fursa hii ili niweze kuuchangia Mswada huu. Kwanza, ningetaka kumpongeza ndugu Sakaja kwa muda aliochukua kuuleta Mswada huu. Mswada huu utawasaidia vijana, hasa kupata kazi na pia kuwaepusha na janga la kuingia kwenye mitego. Kwa wakati mwingi, wakenya wamekuwa wakilalamika kwa sababu ya watu ambao wanawachukua vijana wetu na kuwapeleka Somalia kufanya kazi ya Al Shabaab. Wengine wanapelekwa Saudi Arabia. Wale wanaoenda Saudi Arabia, mwisho wanajuta kwa sababu wanaondoka hapa wakijua wanaenda kufanya kazi fulani na wanapofika kule, wanafanyishwa kazi za nyumbani badala ya kazi ambazo zinahitaji ujuzi wao. Wengine wanaondoka hapa wakijua wanaenda kuwa madereva, lakini wakifika kule, wanapewa kazi za nyumbani. Iwapo tutaupitisha Mswada huu, utawasaidia vijana kwa sababu wote watakuwa wamesajiliwa mahali pamoja. Vile vile, Mswada huu unapendekeza kuwa tuwe na vituo mashinani. Mimi pia, ningependekeza kwamba vituo hivi visambazwe katika maeneo ya Bunge na hata ikiwezekana katika wadi. Tukifanya hivyo, itakuwa rahisi kujua ni nani hana kazi kwa sababu hawa ni vijana ambao tunakutana nao kila tukizunguka. Nina hakika kuwa hali hii itatupunguzia janga la watoto wetu kupotoshwa. Wakati mwingi, vijana wanajiingiza katika anasa za madawa ya kulevya. Utawapata humo vichochoroni wakivuta bhangi na wengine wanaendea “unga.” Wenye kupeana “unga” ni watu ambao wako katika hali nzuri na badala ya kufikiria kama vile mhe Sakaja alivyofikiria na kubuni mbinu hii ya kuona kwamba vijana wa Kenya wanalindwa vilivyo, matajiri wanachukua fursa ya kuuleta “unga” and kufanya ufisadi wa kila aina. Vijana wetu wanakuwa katika hali ambayo hata wao wenyewe hawajielewi. Huu ni uharibifu mkubwa kwa vijana wetu. Ningewauliza wenzangu tuunge mkono Mswada huu ili tuwaepushe vijana wetu na janga ambalo linawakabidhi kwa wakati huu. Kwa hayo machache, naunga mkono."
}