GET /api/v0.1/hansard/entries/561909/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 561909,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/561909/?format=api",
"text_counter": 153,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Gichigi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1909,
"legal_name": "Samuel Kamunye Gichigi",
"slug": "samuel-kamunye-gichigi"
},
"content": "Ninakushukuru Naibu Spika wa Muda. Ninataka kumpongeza Mhe. Sakaja kwa sababu ya kuuleta Mswada huu katika Bunge ili tuwasaidie vijana wetu. Katika Kamati ya Wafanyikazi na Ustawi wa Jamii, tumeongea na Mhe. Sakaja na tumekubaliana kuwa tutafanya mabadiliko kidogo ili tuweke vipengele ambavyo vitashughulikia walemavu pia ili tusiwe na haja ya kuunda shirika lingine la kuwashughulikia walemavu na kina mama. Kwa hivyo, tutaurekebisha Mswada huu ili uweze kuwashughulikia hawa watu wote. Pia, tunataka kuwashughulikia wafanyakazi katika nchi za ng’ambo ili wasiendelee kuumia."
}