GET /api/v0.1/hansard/entries/561959/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 561959,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/561959/?format=api",
"text_counter": 203,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Nakara",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2926,
"legal_name": "John Lodepe Nakara",
"slug": "john-lodepe-nakara"
},
"content": "Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, jambo la kwanza, kuwa na kitengo cha watu hali mahututi katika kila hospitali ya eneo la Bunge ni njia moja ya kuokoa maisha ya watu wetu. Nikipeana mfano kwa sehemu ambayo nimetoka kule Turkana, tunasafiri kilomita 800 hadi mji wa Eldoret kuleta mtu ambaye amepata ajali na ni gharama. Ugatuzi nikupeleka huduma karibu na wananchi. Tukiwa na kitengo cha hali mahututi na cha kutoa damu kwa kila eneo la Bunge ni njia moja ya kupeleka huduma karibu na watu ili watu wapate huduma kwa njia iliyo rahisi kuliko tu kusafirisha watu kutoka maeneo mbalimbali hadi katika hospitali moja ya kaunti mahali ambapo huduma hii inapatikana."
}