GET /api/v0.1/hansard/entries/561960/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 561960,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/561960/?format=api",
    "text_counter": 204,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Nakara",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2926,
        "legal_name": "John Lodepe Nakara",
        "slug": "john-lodepe-nakara"
    },
    "content": "Watu wa Kenya ni wafadhili wazuri. Katika nchi yetu ya Kenya tumebarikiwa na watu walio na mioyo safi. Kuna watu ambao wangependa kutoa damu ili kusaidia wenzao lakini shida ni sehemu ya kwenda kutoa damu hiyo. Kwa mfano, katika kaunti ya Turkana, kuna watu wangependa kuchangia damu lakini mahali pa kuelekeza hao wafadhili ambao wangependa kutoa damu yao ni shida. Kwa hivyo, tukiwa na kitengo kama hiki cha kutoa damu katika kila eneo la Bunge itarahisisha wafadhili ambao wangependa kutoa damu yao kuokoa maisha ya wengine na kupeana kwa haraka. Hii ni muhimu kwa sababu hata kama wewe ni mfadhili, kama huna sehemu ya kupeleka ufadhili wako, inakuwa vigumu kujipa moyo."
}