GET /api/v0.1/hansard/entries/561964/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 561964,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/561964/?format=api",
"text_counter": 208,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Nakara",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2926,
"legal_name": "John Lodepe Nakara",
"slug": "john-lodepe-nakara"
},
"content": "Kuhusu jambo ambalo Mheshimiwa amesema kwamba tuwe katika kila eneo, msongamano mwingi uko katika hospitali ya kaunti kwa sababu ni moja tu. Watu wanasafirishwa kutoka sehemu zote za eneo la Bunge na wanapelekwa katika hospitali moja. Hapo unakuta msongamano katika hospitali hiyo na watu wengine wanapoteza maisha yao kabla hata hawajafikia daktari. Tukiwa na kitengo cha hali ya mahututi katika kila eneo itakuwa rahisi mtu kupata huduma kwa haraka. Kama vile Mheshimiwa Abdul amesema, hospitali zingine za kaunti hazina vitanda. Utakuta wagonjwa wawili ama watatu wakilala katika kitanda kimoja. Kwa mfano, tuliona hospitali za Chuka na Isiolo ambazo ziko katika hali duni. Hali hii inaongeza ugonjwa mwingine ambao mtu hajatoka nao nyumbani. Tungeomba kila hospitali iwe na kitengo cha watu wa hali mahututi na sehemu ya kutoa damu iwe na vifaa vya kisasa ambavyo vinaweza kuokoa maisha ya mwanadamu maana nchi iliyo na afya ni nchi iliyo nzuri. Wakati nchi iko na matibabu mazuri hata watu wa nchi hiyo wanaishi miaka mingi ya kufurahia."
}