GET /api/v0.1/hansard/entries/562069/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 562069,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/562069/?format=api",
"text_counter": 40,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Bw. Spika, wahenga husema: “Mbiu ya mgambo ikilia, kuna jambo. Ndege wengi wakilia, mtafute nyoka.” Leo tunapata watu wa makundi matano tofauti wakipendekeza vilio vyao kwa Bunge hili. Ni mwanzo mzuri ingawa wengine walishafanya hivyo hapo awali lakini tunaona kwamba wananchi wanaanza kutambua umuhimu wa Bunge hili la Seneti. Pia wanatambua kazi yetu. Ibainike, ijulikane na itambulike Kenya nzima, kwamba Bunge hili lina jukumu kuu la kuangalia hasa utu wa Mkenya pamoja na kustawisha na kuangaza mawazo ya usawa. Pia itambulike kwamba hata mahakama imetambua jambo hilo jana, ingawa kidogo ilitunyang’anya nguvu za kuadhibu."
}