GET /api/v0.1/hansard/entries/56304/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 56304,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/56304/?format=api",
    "text_counter": 272,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, kama vile wenzangu waliozungumza mbele yangu wamesema, ingawa pesa zilizotakikana zilipitishwa na mamlaka ya Waziri yemepeanwa kuhusu mafuta yakiwemo ya taa--- Mafuta ya magari ni petroli na diseli na hayana shida sana. Ni jukumu la Waziri kuona kwamba sisi tumehifadhi mafuta ya kutosheleza mahitaji yetu. Pia, inafaa alinde kampuni za hapa nchini zisivurugwe na kampuni za kutoka nje. Kama Shirika letu halitapewa pesa za kutosha ili liagize mafuta, bila shaka tunaweza kudhulumiwa na kampuni za hapa nchini hazitafanya kazi."
}