GET /api/v0.1/hansard/entries/56305/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 56305,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/56305/?format=api",
    "text_counter": 273,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Wenzangu wamezungumzia kuhusu mafuta ya taa. Ninawaunga mkono kwa kusema kwamba wengi wa watu wanaotupigia kura au wengi wa watu tunaowaongoza – bali na kumshukuru Waziri kwa kusambaza stima - wanategemea mafuta ya taa. Mafuta ya taa ni muhimu sana. Mbali na kuwemo kwa soko huru katika kila sekta ya nchi hii, kuna sekta zingine zinazomhusisha mwananchi wa kawaida moja kwa moja. Mafuta ya taa ni bidhaa moja ambayo inamhusu mwananchi wa kawaida. Ningemwomba Waziri afanye vyovyote iwezekanavyo, hata kama ni kuleta Hoja hapa Bungeni, ailete na tuipitishe ili bei ya mafuta ithibitiwe na Wizara ya Kawi. Kati ya asilimia 70 na 80 ya Wakenya ni watu ambao wanahitaji stima, lakini kulingana na kadiri ya mapato yao, hawawezi kamwe kulipa ada ya stima. Kwa hivyo, wataendelea kutumia mafuta ya taa na ni jukumu la Waziri kuhakikisha kwamba bei ya mafuta ya taa imethibitiwa. Vile vile, iwekwe bei ambayo wanaweza kumudu ili waendelee na maisha yao. Wanafunzi wengi wanaosomea nyumbani wanatumia taa zinazotumia mafuta ya taa."
}