GET /api/v0.1/hansard/entries/563052/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 563052,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/563052/?format=api",
"text_counter": 58,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Asante Mhe. Spika kwa nafasi hii. Mengi yamezungumzwa kuhusu suala hili la ardhi ambayo iko Mwatate. Kama ijulikanavyo, ardhi hii ni mojawapo ya dhuluma ambazo zimetendewa watu wa Taita. Kamati imependekeza yafuatayo: Mipaka ya shamba hili ambayo iliwekwa mwaka wa 1992 iregelewe. Soroveya aende apime shamba hilo. Ni sawa na hamna tatizo kama mwenyewe ana ardhi ya ekari 30,000 lakini ardhi yoyote itakayopatikana juu ya ekari 30,000 irudi kwa wananchi wa Mwasima Mbuwa pale Mwatate. Watu wa Mwasima Mbuwa wamelilia ardhi hii na wamejitoa mhanga kuona kuwa haki yao inarudishwa. Kero ni kuwa hata masoroveya wa pale Wundanyi hawawezi kuingia katika shamba hilo. Tunaomba Serikali itumie nafasi hii kuhakikisha kwamba shamba hili linapimwa. La pili ni kuwa bwawa la maji lililoko pale litumiwe na watu wote. Hayo ndio makubaliano yaliyokuweko. Kituo cha polisi kiwe cha umma na watu wote wakitumie. Polisi wasiwe wanatumiwa tu kulinda hali na hadhi ya mwenye shamba ambaye ni Mgiriki. La nne ni kuhusu reli ambayo iko pale. Kituo cha reli ni cha wananchi wa Mwatate. Kifungliwe na kitumike. Tunaomba pia vile vizuizi vya barabara ya kutoka Mwatate kwenda Kasigau ambavyo vimepitia katikati ya shamba vifunguliwe ili barabara hii, ambayo ni ya umma, iwe inaweza kutumika na mtu yeyote bila shida yoyote. La mwisho, naomba ikubalike kuwa suala hili limewakumba Wataita na watu wa Mwatate na wamekaa nalo kwa muda. Tunaomba Ripoti hii, ambayo imeletwa na kamati ya Bunge, ikubaliwe ili mambo haya tuliyoyataja kama vile uwanja wa ndege na msitu wa umma vifunguliwe kwa umma ili umma uwe unaweza kutumia vifaa hivi maana kikatiba ni vyao. Watu wa Mwasima Mbuwa wameonewa. Kwa haya mengi, naunga mkono Ripoti hii na nawasihi Wabunge wenzangu wakubaliane na Ripoti ya Kamati yetu. Asante, Mhe. Spika."
}