GET /api/v0.1/hansard/entries/563059/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 563059,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/563059/?format=api",
    "text_counter": 65,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Lay",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1022,
        "legal_name": "Joyce Wanjalah Lay",
        "slug": "joyce-wanjalah-lay"
    },
    "content": "Vile vile, tukigusia mambo ya mashamba upande wa Mwatate, katika shamba la makonge, limekua na utetezi kwa miaka mingi. Kumekuwa na wananchi ambao wamelia miaka mingi kwa sababu ya kunyanyaswa wakisema ya kwamba shamba hili la huyu bwenyenye ambaye analima makonge pale, ameingilia baadhi ya mashamba ya wananchi. Wamezunguka miaka mingi na ninakumbuka wako na kesi kortini hadi leo. Wamejitolea kuhakikisha ya kwamba haki imepatikana kutokana na kesi hii, lakini nguvu za wananchi ni chache kuliko za aliye na pesa nyingi. Akienda kortini, kuna njia anazotumia kuhakikisha haki ya wananchi haitendeki. Kulingana na Ripoti iliyosomwa mbele yetu, kuna barabara ambazo zimefungwa ili wananchi wasitumie ilhali ni za umma. Kisheria and hata kikatiba, hawa wananchi wa Taita Taveta upande wa Mwatate wamenyanyasika kwa miaka mingi. Hili ni jambo ambalo lazima liangaliwe."
}