GET /api/v0.1/hansard/entries/56306/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 56306,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/56306/?format=api",
"text_counter": 274,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, vile vile, ningependa kumshukuru Waziri kwa kumteua Mkurugenzi wa National Oil Corporation of Kenya (NOCK). Kulikuwa na mtafaruku kuhusu uteuzi huo na Waziri amechukua hatua hiyo na sasa hivi tuna Mkurugenzi katika Shirika la NOCK. Wizara ya Kawi inatakikana ihakikishe kwamba inasaidia miradi ya stima katika kila sehemu ya uwakilishi bunge kwa sababu ina uwezo wa kufanya hivyo. Kama ni mambo ya elimu, inafaa yasiachiwe Wizara ya Elimu pekee. KenGen inapata pesa nyingi kutoka kwa wananchi. Kwa hivyo, shirika hili linaweza kujenga vyuo, vituo vya matibabu au shule hata kama ni ya nasari."
}