GET /api/v0.1/hansard/entries/563075/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 563075,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/563075/?format=api",
"text_counter": 81,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Shukrani, Mhe. Spika. Nasimama kuunga mkono Ripoti hii ambayo imetolewa na Kamati ya Ardhi na pia kuipongeza kwa maana kwa muda tuliokua nao, wameweza kuzunguka katika maeneo mengi wakijaribu kutatua haya mambo ya ardhi. Naiunga mkono hii Ripoti kwa sababu ukiangalia kiundani, utaona kwamba hili eneo la Taita ni moja kati ya maeneo ya Pwani ambayo yamedhulumika sana na mambo ya ardhi. Ikiwa tutaweza kuyafuatilia unyo unyo kama vile ilivyo saa hizi, nina imani tutaweza kuweka roho za wananchi katika hali ya usalama na kuweka roho za wananchi katika imani ya kuamini kwamba walichagua viongozi wanaowajali."
}