GET /api/v0.1/hansard/entries/563079/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 563079,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/563079/?format=api",
    "text_counter": 85,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 751,
        "legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
        "slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
    },
    "content": "Pia, Kamati ya Ardhi iangalie kwa kina, katika wale ambao wanagawanya ardhi, kuna wengine ambao wanatumia ulaghai. Wanajihesabu kuwa wao ni maafisa wanaokuja kusaidia na kumbe palepale wanajikatia visehemu vyao. Tungependa kuona mkono wa sheria ukifanya kazi ili tuweze kuondoa tatizo hili sugu ambalo limetukabili haswa katika maeneo yetu ya Pwani. Tumeumia na mpaka sasa hatuna cha kujivunia. Hii ni hatari kubwa kwa sababu tumewahi kumwaga damu kwa sababu ya mambo ya ardhi. Hatutaki kuona tena nchi yetu ya Kenya tukipigana kwa sababu ya ardhi. Tunataka tupigane na tumbo, ukosefu wa kazi na mambo ya usalama, lakini siyo kwa mambo ya ardhi. Pia, tutakapokuwa tumetatua haya mambo ya ardhi, tutaweza kuondoa yale ambayo yamekuwa yakitumiwa na wanasiasa kutafuta kuchaguliwa. Tunataka mambo ya ardhi yatatuliwe ili tuweze kubaki katika maeneo yetu na tufaidike kama Wakenya wengine. Shukrani sana. Ninaunga mkono hii Ripoti."
}