GET /api/v0.1/hansard/entries/563103/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 563103,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/563103/?format=api",
    "text_counter": 109,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Nassir",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": "Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Maswala ya ardhi kama nilivyosema yameweza kumwaga damu katika sehemu nyingi za Kenya. Kenya iliweza kupata Uhuru wake na jambo kubwa zaidi lilikuwa ni kuhusiana na maswala ya ardhi. Idadi ya Wakenya sasa hivi inazidi na kiwango cha ardhi ni kile kile. Dhuluma ambazo ziliweza kufanywa katika kihistoria hususan sisi kama watu wa Pwani, tusipoweza kuanza kuzitatua sasa hivi---Karne hii isipoweza kuwa ndio ya kutatua shida za ardhi zilizokuwa ziko, basi hatari yake itakuwa ni kubwa zaidi."
}