GET /api/v0.1/hansard/entries/563111/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 563111,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/563111/?format=api",
"text_counter": 117,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Nassir",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": "Nikimalizia nilikuwa nazungumza kuhusiana na maswala ya ardhi katika eneo Bunge langu la Mvita. Mabwenyenye walioridhi ardhi wanasemekana ni wenye ardhi zile licha ya kuwa hawaonekani. Kuna watu wamekuwa wakilipa ada na kodi za ardhi kwa muda wa miaka na ikipigwa hesabu ya kodi ambazo wameweza kulipa pale na dhamani waliyoweza kuiweka katika ardhi ile, hivi sasa itakuwa ile ardhi kisawasawa inastahili kuwa ni yao. Nashukuru Mungu ya kuwa tume inayosimamia mambo ya mashamba imekubali kuja katika eneo Bunge la Mvita na kuweza kukaa chini pamoja na kila mitaa na watu waweze kuwaelezea shida za ardhi ambazo zinawakumba. Ningeomba maeneo mengine yaweze kuiga mfano ili historia iweze kutuhukumu ya kuwa Bunge hili ndilo ambalo limeweza kutatua lile donda sugu la ardhi."
}