GET /api/v0.1/hansard/entries/563115/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 563115,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/563115/?format=api",
    "text_counter": 121,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Kenya hii, wananchi wamekuwa wakipigana na kugombana kwa sababu ya swala hili ambalo limetatiza Wakenya sana. Baada ya Katiba iliyopitishwa mwaka wa 2010, haswa wale ambao walikuwa na matatizo ya kihistoria kama yale maeneo tunayotoka sisi, sasa hivi tutapata afueni kama Kamati ya Bunge ya Ardhi itaendelea na kazi hii ambayo imekuwa ikifanya. Huku nchini kuna watu ambao kazi zao nyingi haswa nikiangalia upande wa Taita Taveta ni kupita wakidanganya wananchi ili kuwakoroga akili na hata ile kazi ambayo inafanyika inakuwa shida sana kuweza kutekelezwa. Hivyo basi, Wabunge, viongozi ambao wamechaguliwa mashinani, wakitekeleza majukumu yao namna hii, tutaweza kuyamaliza matatizo ambayo yanatukabili hapa nchini haswa maswala ya ardhi. Mheshimiwa Spika wa Muda, wananchi wanaokaa upande wa Mwatate wameteseka sana. Ukiangalia, utaona kuwa wamepandiwa makonge hadi mlangoni. Kwenye Ripoti hii, The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}