GET /api/v0.1/hansard/entries/563117/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 563117,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/563117/?format=api",
    "text_counter": 123,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Vile vile nikitaja maswali ya Taveta, ninataka kutoa shukrani kwa Serikali ya Kenya kwa kutoa ekari 5,000 ili Wakenya wanaoishi Taveta, haswa Wataveta, wapewe maeneo yale. Ni kweli kuwa wananchi pale walitarajia kuwa zile jamii mbili au tatu ambazo zinaishi pale ndio pekee wangepatiwa shamba lile. Lakini tukiangalia, sheria ilifuatwa na tukahakikisha kuwa wote, hata wale ambao walikuwa kwenye vijiji kwenye hilo shamba, wamepatiwa mashamba na haswa wakapatiwa vyeti vya kumiliki ardhi isipokuwa wengi wao walidanganywa hata wakauza mashamba yao kwa sababu waliambiwa kuwa vyeti hivi si vya ukweli. Hiyo yote ni ile propaganda iliyopitishwa pale na wale ambao wameendelea kufanya hivyo. Wabunge walipoenda kule, waliambiwa kuwa hata wale ambao walikuwa na malalamishi walipatiwa vyeti vyao vya kumiliki ardhi. Hivyo basi, bila shaka, sina wasiwasi kuwa Tume ya Ardhi nchini ikifika pale, itaona kuwa kila kitu kimefanywa sawa. Ningetaka pia kuishukuru Tume ya Ardhi kwa sababu tayari, walikuwa wametembea Taveta na bado watarudi ili kuhakikisha kuwa wananchi wameingia kwa mashamba yao. Ninaunga mkono Ripoti hii."
}