GET /api/v0.1/hansard/entries/563881/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 563881,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/563881/?format=api",
"text_counter": 146,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ninamuunga mkono ndugu yangu, Sen. Abdirahman. Hata hivyo, ninataka ajue ya kwamba sio tu kwamba hatuna walimu waliohitimu; wapo. Hivi leo tukiandika walimu, utaenda katika kila kaunti na utakuta watoto wetu wamebeba stakabadhi na wanalia machozi wakitaka kuandikwa kazi. Wanachoambiwa ni kwamba hakuna pesa za kuwalipa kisha wanarudi nyumbani. Shule hazina walimu lakini watoto wetu waliohitimu kwa ualimu wanarudi nyumbani. Hivi sasa ndugu yangu anataka hata tuandike wale ambao hawajahitimu ualimu. Kwa sababu gani? Tunaona hao ndio wanaweza kufanya kazi kwa sababu wataona ni kama bahati imewaangukia. Kama hawajahitimu na wapewe hiyo kazi, wataona ni rahisi kuingia na kufanya ile kazi. Bw. Spika wa Muda, ikiwa Serikali ya Jubilee haitaweka pesa katika elimu, ujambazi hautapungua. Niliona jana mhe. Rais alienda nyumbani kwake na kujaribu kutilia mkazo kwamba watoto waache kunywa pombe haramu. Nilimwona mhe. Mhe. Rais akitabasamu na kuongea vizuri akisema kwamba pombe hiyo ni haramu na ivunjwe jamii. Baada ya kuzungumza hayo yote, aliwapa hao vijana aliohutubia mwelekeo na tegemeo gani kwamba kama hawatakunywa hiyo pombe na kulala hoi, akili zao zitakuwa katika hali ya kufikiria na hawatapata nafasi ya kunywa pombe? Tumesahau kwamba wanaokunywa pombe hiyo hawanywi kwa hiari yao bali ni kwa kutaka kukandamiza na kuondoa mawazo ambayo yanawaelekeza kufanya mambo machafu. Tunapofanya mikutano kama ya jana, kazi yetu ni kulaumu kwamba hii inauzwa na haifai, tunataka muache pombe na muwe vijana wazuri. Unamwambia mtu ambaye ana mke na ana njaa na shida aache kunywa pombe na akifika nyumbani, mke anamwuliza chakula na watoto pia wako hapo, halafu akili yake inatakiwa kuwa timamu? Mhe. Rais aangalie kitakachotoa mambo haya na kuwawezesha vijana hawa kuendelea na maisha ya kawaida. Nikimalizia, ninasema kwamba pesa ziende kwa wananchi ili tutekeleze majukumu ambayo yatasaidia watoto wetu. Viongozi wa nchi hii wametajirika vya kutosha. Ninaona tunaelekea kiwango ambacho mhe. Rais atatoroka nchi hii, na aende katika nchi ya nje kama Mobutu, ndio adhabu ipatikane hapa. Bila hayo ---"
}