GET /api/v0.1/hansard/entries/563883/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 563883,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/563883/?format=api",
"text_counter": 148,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, ningetaka kurudia yale nilikuwa ninasema; mpaka siku mhe. Rais aliyeko madarakani iwe ni sasa ama siku zijazo aandamwe na wananchi na wamlazimishe afanye yale wanayoyataka. Inafaa aingiliwe vilivyo hadi anyanyue mbio. Hivyo atakuwa ameweka rekodi ya kusema kwamba kama hutendi yale matendo yanayofaa, Wakenya hawatakupatia nafasi. Labda nimejielezea kwa lugha ngumu kidogo, lakini hivyo ndivyo nilivyomaanisha. Inafaa Wakenya walalamike wazi wazi na kukataa kutendewa maovu. Ni dhahiri kwamba mhe. Rais wa kwanza wa Taifa letu la Kenya ndiye aliyemiliki mashamba makubwa zaidi. Mhe. Rais wa pili ndiye anayemfuata, na mhe. Rais wa tatu anawafuata. Huyu wa nne anakalia yale mashamba ya babake. Hatusemi kwamba ni mwananchi wa kawaida ndiye anayetenda vitendo hivi; ni wale walioko kwenye mamlaka. Ndio maana ninasema kwamba viongozi katika nchi hii wametajirika vya kutosha. Hivi sasa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}