GET /api/v0.1/hansard/entries/563891/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 563891,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/563891/?format=api",
"text_counter": 156,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna chanzo cha kila tatizo. Tatizo halitokei bila sababu. Hivi leo shida ya nchi yetu ni uharibifu wa mali ya Wakenya na mpangilio mbaya ambao pesa zinachukuliwa na kuwekwa pahali itatoa marupurupu. Tunapoongea juu ya matatizo haya, hatuwezi kukosa kusema kwamba chanzo cha matatizo haya ni uongozi mbaya. Ni nani anayebeba msalaba wa kutoa uongozi mwema na kujaza pengo la mahitaji ya Wakenya? Ni sisi viongozi. Watu wasikubaliwe kufanya wanavyotaka katika nchi hii bila kushtumiwa. Hatuwezi kusingizia kuwa Hoja hii ni juu ya waalimu, kwa hivyo tusiongee mambo mengine ila tu kumshtumu Bw. Sosion, kwa sababu anatetea maslahi ya waalimu kulipwa mishahara mizuri ilhali hatutaji wale wanaoiba pesa hizo. Tunataka kusimama katika uongozi dhahiri na uliyo wazi. Chanzo cha mambo haya ni kwa sababu tumekuwa na uongozi mbaya. Tunaweka pesa mahali ambapo hapafai. Bw. Naibu Spika wa Muda, anakotoka Sen. Abdirahman---"
}