GET /api/v0.1/hansard/entries/566421/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 566421,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/566421/?format=api",
"text_counter": 145,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Mumo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 808,
"legal_name": "Rose Museo Mumo",
"slug": "rose-museo-mumo"
},
"content": "Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nashukuru kwa kunipa nafasi hii. Ningependa kuchangia jambo hili la kupata benki ya damu, ama kupata hiyo transfusionservice – Kiswahili kinanipungukia kidogo – ni jambo muhimu na la maana sana katika kaunti zetu. Kile ningesema ni kwamba, kuanzisha chumba cha wagonjwa mahututi ni jambo muhimu sana. Hata hivyo, tuangalie kama tuna sifa, ujuzi na mambo ambayo yanatuwezesha kuanzisha vyumba hivi. Kuanzisha jambo hili katika kila eneo la uwakilishi Bungeni ni vigumu. Ni vigumu kwa sababu gani? Ni vigumu kwa sababu hakuna mahali ambapo tumeanzia. Ni lazima tuanzie mahali maanake hata tukiangalia hospitali nyingi hapa Nairobi ni chache sana zilizo na vyumba vya kuangalia watu mahututi. Jambo lenyewe ni jema kwa sababu akina mama wengi wanapoteza maisha yao wakati wanapojifungua. Unakuta kwamba hakuna damu ya kuwapa kwa maana wanavuja damu nyingi; kama tungekuwa na damu ama njia ya kuwapa akina mama hawa damu, tungeokoa maisha ya wengi wao. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}