GET /api/v0.1/hansard/entries/566422/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 566422,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/566422/?format=api",
    "text_counter": 146,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Mumo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 808,
        "legal_name": "Rose Museo Mumo",
        "slug": "rose-museo-mumo"
    },
    "content": "Jambo lingine ni kwamba katika eneo la uwakilishi Bungeni au Kaunti ya Makueni ambayo mimi ninatoka, sehemu kubwa inapitiwa na barabara ya Mombasa ambapo kunatokea ajali nyingi sana, na maisha mengi hupotezwa. Hii ni kwa sababu watu wanapopata ajali pale, wengi hupoteza damu na inakuwa ni vigumu kupata nyingine ili wasaidike kimaisha. Kama tungeweza kuwa na huduma hizi katika kaunti zetu, wengi wa watu hawa ambao hupoteza maisha yao wangeokolewa kwa kupata damu kwa haraka. Lingine, ninapomalizia, ni kwamba utekelezaji wa jambo hili ungekuwa ni wa haraka iwapo tungelianzisha katika kaunti kuliko kusema tuazishe katika kila eneo Bunge. Tunaweza kuzungumza hapa tu lakini iwe vigumu na ichukue miaka mingi wakati maisha ya wengi yakipotea. Ningeomba tufikirie kuanzisha katika kaunti ndipo tuangalie jinsi uwezo wetu utapatikana kuanzisha katika kila eneo Bunge baadaye. Tuangalie jambo linaloweza kutekelezwa na lisiloweza kutekelezwa. Nashukuru na naunga sana mkono jambo hilo la kupata na kupeana damu katika kaunti na pia kuanzisha vyumba vya wagonjwa mahututi. Asante."
}