GET /api/v0.1/hansard/entries/566424/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 566424,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/566424/?format=api",
    "text_counter": 148,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. S.A. Ali",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ya kuchangia Hoja hii. Vilevile ningependa kumpongeza Mheshimiwa ambaye ameleta Hoja hii baada ya kuzingatia pakubwa suala la afya katika nchi yetu. Kwa kweli hii ni Hoja ambayo inaonekana ni kama imeletwa Bungeni kama Hoja nyingine za kawaida, lakini ukweli ni kwamba suala la afya katika nchi hii limeachwa nyuma sana na limekuwa katika hali ya kutothaminiwa. Mjadala uliopo ni baina ya kauli mbili: Je, huduma hii ipatikane katika kaunti au katika maeneo Bunge? Kwa kweli ni jambo la kusikitisha. Hivi sasa huduma hii haiwezi kupatikana katika baadhi ya kaunti hata ingawa tuna miaka 52 ya Uhuru. Hilo ni jambo la kusikitisha. Kuna umuhimu mkubwa nchi hii kuzingatia suala hili kwa sababu kifo kimewekwa na Mwenyezi Mungu. Sababu kubwa ya watu kufariki ni kutokuwa na huduma bora katika sehemu nyingi katika nchi hii. Tukizungumzia huduma hizi kuwepo katika kaunti, hata zikiweko katika kaunti, mgonjwa anapotolewa mahali anapotoka kukimbilia mahali huduma hii inapatikana, kuweza kufikia huduma hii, kulingana na hali ya barabara zetu wengi wanakufa katika magari ya kubebea wagonjwa kwa sababu ya misongamano ya magari katika barabara zetu. Suala hili lahitaji kuzingatiwa pakubwa. Kuna umuhimu mkubwa kila mwananchi katika nchi yetu ya Kenya kuhakikisha ya kwamba amepata huduma ya kawaida. Watu wengi sana hawawezi kujimudu kwa sababu ya matatizo ambayo tuko nayo. Ni muhimu kuhakikisha kwamba kila mwananchi anayeishi katika Kenya hii amehudumiwa. Wakenya wengi wanasafiri nchi za nje kwa sababu suala hili la afya huonekana ni kama halina thamani ama halitiliwi juhudi katika nchi yetu. Siyo kwamba hatuna watu wa kuhudumia wagonjwa. Mipangilio katika Serikali yetu ya kuliendesha jambo hili ndiyo inaleta pingamizi kubwa katika kulifanikisha jambo hili. Uwajibikaji ni jambo muhimu sana. Leo hii tunazungumza kuhusu kuweka huduma hizi katika maeneo yetu ya Bunge, lakini ikiwa hakutakuwa na uwajibikaji, itakuwa ni kama vile Waswahili husema, kumpigia mbuzi debe. Kuna dharura kubwa ya kuwajibikia masuala haya. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}