GET /api/v0.1/hansard/entries/566425/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 566425,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/566425/?format=api",
    "text_counter": 149,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. S.A. Ali",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Wakenya wanaumia. Ni lazima iwapo tumekubaliana kupitisha mambo kama haya, ufuatilizaji na uwajibikaji ni lazima upatikane kwa sababu tunaweza kuyapitisha mambo haya lakini yakabaki vilevile kwamba hayana maana yoyote kama inavyosemwa na wenzangu. Inaonekana ni kama ndoto tunajaribu kupanga hivi sasa. Lakini ninaamini pakubwa hakuna jambo ambalo haliwezekani. Utapata kwamba, kwa mfano, hapa tulipo wakati mmoja palikuwa ni kiwanja tu. Waliofikiria kujenga Jumba hili walikuwa na mpango wakalijenga. Hivi sasa tukisema tutatoa huduma hizi sharti tuhakikishe kwamba kila mmoja amewajibika katika kulitekeleza jambo hili. Hivi sasa tumepeana majukumu ya afya kwa serikali za kaunti. Ingawa hivyo kuna malalamishi mengi.Ni kwa nini? Tatizo liko wapi? Limesababishwa na nini? Tatizo kubwa ni kutowajibika. Je, hakuna pesa za kuendesha shughuli hii? Katika kaunti yangu ya Lamu, hakuna huduma hizi. Tujiulize kosa liko wapi. Matatitzo yako wapi? Ikiwa ni pesa, Serikali kuu inapeana pesa kwa Kaunti ya Lamu. Je, ni viongozi walioko pale hawajawajibika kuliangalia suala hili? Anayeumia ni nani? Mwananchi wa kawaida anaenda sehemu nyinginezo kutafuta hizi huduma. Tukisema kwamba tutaweka katika kituo kimoja katika kaunti---"
}