GET /api/v0.1/hansard/entries/566450/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 566450,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/566450/?format=api",
"text_counter": 174,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Katana",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 691,
"legal_name": "Aisha Jumwa Katana",
"slug": "aisha-jumwa-katana"
},
"content": "Asante sana Mhe. Dawood, ama Mhe. Naibu Spika wa Muda ndiye amenipa nafasi. Nataka nichukue nafasi hii kwanza nimpongeze sana Mhe. Dawood pia kwa kunipatia dakika yake moja ili nipaze sauti yangu kuhusu Hoja hii. Nimesimama kuiunga mkono. Nataka kwanza nipongeze pia lile jopo la wataalam ambalo lilikuja na mabadiliko ijapokuwa yameangushwa; niliomba sana wenzangu tuyazingatie kwa sababu maswala ambayo yamezungumzwa ni ya ukweli ili kuhakikisha swala hili limepata uhakika wa kufanyika, na ni lazima tulizungumze kwa upana. Kupata ICU katika kila eneo la uwakilishi Bungeni una ugumu kama vile wenzangu waliotangulia kusema. Pia kuna umuhimu sana watu kuzingatia huduma hii. Kwa mfano, wakati huu katika shughuli ya uchukuzi tuna wale vijana wetu wanaoendesha boda boda na ajali zimekua nyingi sana katika sehemu zetu."
}