GET /api/v0.1/hansard/entries/566588/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 566588,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/566588/?format=api",
"text_counter": 312,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwashetani",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2163,
"legal_name": "Khatib Abdallah Mwashetani",
"slug": "khatib-abdallah-mwashetani"
},
"content": "Wabunge 11, magavana wawili na wawakilishi 85 katika mabunge ya kaunti. Kama si maelewano na Chama Kikuu cha Orange Democratic Movement (ODM), sisi tungekuwa katika hali mbaya kwa sababu ni muhimu uwakilishi ufike mashinani. Na kufikisha uwakilishi mashinani, ni lazima kuwe na pesa za kuwalipa maafisa na wale ambao wanasambaza jina la chama. Mhe. Naibu Spika wa Muda, naunga mkono Mswada huu ili pesa hizi ziwafaidi Wakenya wote. Vile vile, hizi ni pesa za umma ambazo zinafaa kufika kwa wananchi wote nchini Kenya. Pesa hizi za umma zina haki kutambulika na kujulikana jinsi zinatumika. Ikiwa zitakwenda katika vyama, tunaweza kubuni sheria mwafaka na vile vile kuandikisha vyama vipya. Nitapinga yale maneno ambayo yamezungumziwa - kwamba iwapo tutayapitisha marekebisho hayo, basi vyama vingi zaidi vitaandikishwa. Kuna tetesi kwamba vyama vitakavyosajiliwa vitakuwa vingi kushinda vile vilivyoko hivi sasa. Sioni kama tetesi hiyo ni sawa kwa sababu tayari sheria ya kuandikisha vyama iko, na imeweka mikakati ili kuchuja vile chama ambavyo vitakuwa na mwelekeo wa kisawasawa. Kwa hayo machache, naunga mkono Mswada huu."
}