GET /api/v0.1/hansard/entries/566609/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 566609,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/566609/?format=api",
"text_counter": 333,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kombe",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 250,
"legal_name": "Harrison Garama Kombe",
"slug": "harrison-kombe"
},
"content": "Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Naunga mkono Mswada huu kwa sababu hata vyama vidogo vinachangia katika uchumi wa nchi hii. Ukiwa na watoto na uanze kuwabagua na kusema: “Huyu anatambaa, hastahili kupata huduma kutoka kwangu; nitahudumia yule ambaye tayari yuko mbio kujitafutia”, hapo husaidii. Itakuwa ni busara kwetu ikiwa wakati wa marekebisho ya mwisho tuseme kwamba chama chochote kitakachokuwa na mwakilishi Bungeni kifadhiliwe kwa sababu kimeweza kuweka kiongozi Bungeni kupitia kwa wanachama na wananchi ambao pia wanachangia hela za kuendeleza hivi vyama na hata nchi. Tukisema hivi vyama vidogo havistahili kupata huu mgao, tunajaribu kuvunja demokrasia. Tunataka uwazi na nafasi kubwa ya demokrasia ionekane katika nchi hii kwa kuvipa nafasi vyama vidogo vidogo fedha. Nakumbuka mwaka wa 2002 nilikuwa Mbunge wa pekee wa Chama cha Shirikisho. Ni hali ngumu kwa mtu mmoja kufadhili chama mpaka kifikie wakati wa uchaguzi mwingine. Ni shida kukifadhili chama. Hivyo basi, ni vyema kwamba chama chochote kilicho na Mbunge kifadhiliwe. Kwa hayo machache, Mhe. Naibu Spika wa Muda, naunga mkono Mswada huu."
}