GET /api/v0.1/hansard/entries/566779/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 566779,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/566779/?format=api",
    "text_counter": 145,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Bw. Spika, nimesikiza taarifa iliyotolewa na Naibu Mwenyekiti. Ningependa kumjulisha na kumkosoa kwamba shida ambayo inakabili Kaunti ya Kitui inahusu makabila mawili; Wasomali na Wakamba. Ni dhahiri kwamba hatua zilizochukuliwa zinatenganisha makabila haya mawili. Ikiwa watu wa Kitui watachukua hatua, itaelekezwa kwa Wasomali kisha itakuwa vita vya kikabila. Inafaa Naibu Mwenyekiti afahamu kwamba chochote kitakachotokea ni vita vya makabila. Ikiwa vitaanzia Kitui, vitaenea taifa nzima. Kwa nini Serikali haichukui hatua madhubuti kuhakikisha kwamba matendo haya yanasimamishwa haraka iwezekanavyo?"
}