GET /api/v0.1/hansard/entries/566909/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 566909,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/566909/?format=api",
    "text_counter": 275,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, ni matumaini yangu kwamba mhe. Rais wa taifa hili atapokea ujumbe tunaotuma kwa sasa. Serikali ya Jubilee ina jukumu la kulinda maisha ya Wakenya. Tangu Jubilee iingie mamlakani, tumeshuhudia maafa ya Wakenya ambao hawana hatia. Juzi Wakenya walishuhudia mhe. Rais katika mkutano wa kumaliza pombe haramu akinyosha kidole na kusema: “Wewe fulani ninakuagiza hivi sasa ufanye msako mkali kabisa.” Anayeambiwa mambo hayo, juu yake kuna Mkuu wa Polisi. Mhe. Rais mwenyewe anaruka kitengo cha uongozi na kupeana amri kwa askari wa mamlaka ya chini ambaye anasimamiwa na Mkuu wa Polisi. Ni Mkuu wa Polisi ambaye anasatahili kutoa amri bali si Mhe. Rais. Mhe. Rais hata hafai kutaja majina na kusema, askari fulani ndiye atafanya kazi. Huyo Mkuu wa Polisi atawezaje kufanya kazi kwa uaminifu na heshima ikiwa askari wake wa chini ndio wanatumwa kwenda kufanya kazi ya ukaguzi wa pombe? Bw. Spika wa Muda, Serikali ya Jubilee imetumia rasilmali ya nchi hii kwa mambo ambayo hayafai. Mimi ninakumbuka mwaka uliopita tukiwa na shughuli za Saba Saba wakati Serikali ya Jubilee ilituma askari 15,000 kupambana na watu ambao hawakuwa na silaha hata moja. Hii Serikali ya Jubilee imetumia askari kupambana na pombe haramu. Lakini wananchi wanapouawa kule Mandera ambako watoto hawasomi, mhe. Rais anakaa akitabasamu na kucheka bila wasiwasi. Hata mhe. Naibu Rais anaenda kanisani na kuongea mambo ya wokovu na kusema kwamba Kenya ina amani. Amani gani ikiwa watoto wa Mandera hawaendi shule ilhali watoto wao wanatabasamu na kufurahi? Ni Serikali gani itawalinda hawa wananchi maskini ikiwa Serikali ya Jubilee haiwezi kuwalinda? Hivi sasa tunapoongea inakisiwa kwamba zile pesa tulizotengea Wizara ya Ulinzi zinaingia katika mifuko ya watu binafsi. Hivi juzi, badala ya Serikali hii kuzungumza juu ya mambo ya ulaghai unaotokea katika nchi hii, wanaenda kumtetea Bi. Anne Waiguru kule Ikulu. Huyu ni mtu ambaye ameiba na anatakiwa kukomeshwa. Badala ya kutumia hiyo nafasi kutetea Wakenya wanaopoteza maisha yao, Msemaji wa Ikulu anamtetea---"
}