GET /api/v0.1/hansard/entries/566921/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 566921,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/566921/?format=api",
"text_counter": 287,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, mambo yanayotokea katika nchi yetu ni mambo ya kuudhi sana. Wananchi wakiwa wanauwawa bila hatia ilhali Serikali ya Jubilee inapanga kutumia pesa ambazo hazijapitishwa na Bunge kujenga ukuta mipakani wa Kenya na Somalia. Vijana wetu hawana kazi, watu wanauwawa lakini wanataka kujenga ukuta huku wakipora pesa. Wananchi Wakenya tunasema kwamba serikali yoyote ambayo haiwezi kulinda maisha ya wananchi wake haistahili kuwa katika uongozi. Hivi sasa tunaongea kwa majonzi. Mtu yeyote ambaye anasimama hapa na kupinga mambo haya, hata yeye ni muuaji. Hii ni kwa sababu hakuna mtu ambaye atapinga mauaji yakizungumziwa na kuleta siasa za sera ya chama hapa, huku akisema kwamba anatetea Serikali. Wanaosimama hapa na kupinga, ingelikuwa ni watoto wao ama wajukuu wao, makanisa yote Jijini Nairobi yangekuwa yamejaa na watu wenye vitambi vikubwa, magari makubwa na suti za pesa nyingi wakiomboleza."
}