GET /api/v0.1/hansard/entries/566934/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 566934,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/566934/?format=api",
    "text_counter": 300,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Haji",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 26,
        "legal_name": "Yusuf Mohammed Haji",
        "slug": "yusuf-haji"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, hili ni jambo la kusikitisha sana. Jambo hili linatufanya tuzubae hata tukakosa la kusema. Hii ni kwa sababu mara nyingi tumesikia – katika hii Seneti na mikutano – Wakenya wakizungumza juu ya ukosefu wa amani katika nchi yetu. Tunafaa kuweka siasa kando na kusema ukweli. Ni lazima mambo ya amani yachunguzwe na kuangaliwa kwa makini na mtu yeyote anayejali maslahi ya Wakenya na anayependa nchi yake kama sisi tunavyoipenda nchi yetu. Mbali na yale ambayo yametokea Mandera na sehemu zingine za nchi, ni juzi tu ambapo kulikuwa na Hoja hapa kuhusu maafisa wa Shirika la Wanyama Pori (KWS) kuua watu kiholela katika mbuga za wanyama. Imesemekana kuwa watu wasio na hatia yoyote wameuwawa na wengine kupigwa risasi huko Mount Elgon. Hali hiyo inaleta wasiwasi kubwa. Kutoleana lawama hakutatusaidia. Ni lazima tuweke vichwa vyetu pamoja na kuona kile ambacho tunaweza kufanya ili tusaidiane kurudisha amani katika nchi yetu. Wakati mmoja, Rais alizungumza na wakuu wa wilaya ambao siku hizi wanajulikana kama county commissioners. Vile vile, alizungumza na county policecommanders. Aliwaambia kuwa kutokana na ukosefu wa amani, hawezi kukosa usingizi kwa sababu hawafanyi kazi yao. Aliwaambia kuwa ikiwa wangemkosesha usingizi, hata wao wangeukosa. Bw. Spika wa Muda, wakati Bw. ole Lenku aliondolewa mamlakani, nilisema hapa kuwa yeye wala mhe. Rais hawakuwa na hatia yoyote. Hakuna mtu yeyote anayetarajia mhe. Rais kuchukuwa bunduki na kwenda kuchunga watu. Kuna watu walioajiriwa kufanya kazi hiyo. Wanapewa mishahara na silaha ili kulinda wananchi wa Kenya. Bw. Spika wa Muda, jambo lililotokea huko Mandera haliwezi kusamehewa hata kidogo. Hatufai kuwafuta kazi wakubwa wote wa huko. Wanafaa kupelekwa kortini kwa sababu hii ni mara ya tatu watu kuuawa kiholela na kinyama. Watu waliotoka sehemu zingine za nchi kwenda kutafuta riziki ya watoto wao huko Mandera waliogopa kukaa mbali na wenzao. Walikodisha nyumba zilizo pamoja ili waishi kwa amani na kuhisi kuwa wana usalama wa kutosha. Je, kama kuna askari 600 katika sehemu hiyo, mbona Serikali haikutenga askari kumi wa kuwachunga hawa watu kwa masaa 24? Ni uzembe na ukosefu wa imani na kupenda nchi yetu. Wanaweka tamaa mbele ya kuhakikisha kuwa kuna usalama. Siwezi kuwalaumu Kamishna wa Polisi wala Mkurugenzi wa Ujasusi kwa sababu wanawategemea maafisa---"
}