GET /api/v0.1/hansard/entries/566962/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 566962,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/566962/?format=api",
"text_counter": 328,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Ningependa kumshukuru ndugu yangu, Seneta wa Mandera, kwa kuleta Hoja hii. Jambo la kwanza ni kusema ni pole kwa wale wote waliofiwa pamoja na jamii zao huko Mandera. Pia nawapa pole kubwa kwa Wakenya ambao wamepoteza maisha yao. Jambo la kwanza ambalo ningependa kusema ni kwamba Katiba inasema kinagaubaga kuwa maisha ya Wakenya yako juu ya mikono ya mhe. Rais. Hilo ni jambo ambalo hatuwezi kulitoroka. Katiba ni sheria kuu ya nchi hii. Mhe. Rais hawezi kuepukana na jukumu hilo. Kila mkenya yafaa alindwe na mhe. Rais katika maisha yake. Hivi sasa tusiseme kwamba tushirikiane hivi ama vile, yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Kenya. Kwa hivyo ikiwa Wakenya wanakufa hivyo ni jambo la kusikitisha. Tunasikia Wakenya wamekufa Baragoi, Mandera, Wajir na kwingineko. Swali ni, polisi wako wapi? Bw. Spika wa Muda, kwa nini watu wanaoua wengine hawashikwi na kupelekwa kortini? Kwa nini sisi kama Wakenya hatuwezi kujiuliza ni kwa nini watu wanauana katika Kenya yetu ya leo? Hata sisi hapa ndani hatuna hakika ya kwamba tutaona kesho kwa sababu huko nje hatujui nani anatungoja. Huwezi kuwa na imani katika nchi ikiwa hujui maisha yako yanaweza kutetewa vipi. Tumepewa mifano ya kwamba huwezi kumshika Mwamerika leo na kumpeleka katika korti nyingine. Watakwambia umpeleke kwa korti ya Marekani. Ni aibu kwa Kenya ya leo kwamba Naibu wa Rais anapelekwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai na kushitakiwa ilhali sisi hapa tunamuita mhe. Naibu wa Rais. Jambo la kwanza, ni lazima tuzingatie ukenya an uzalendo wetu. Ni lazima mhe. Rais achukue jukumu la kutetea maisha ya kila mtu katika Kenya. Mwanzo tulikuwa tunasema tunajivunia kuwa Wakenya. Baadaye, tukaanza kusema kwamba tunavumilia kuwa Wakenya. Hivi sasa ukiniuliza mimi nitakwambia naogopa kuwa Mkenya. Huwezi hata kidogo--"
}