GET /api/v0.1/hansard/entries/567315/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 567315,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/567315/?format=api",
    "text_counter": 340,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Asante, mhe. Spika. Nashukuru kwa kupata nafasi hii kutoa mchango wangu kuhusu Hoja hii. Kwanza, ningependa kumpongeza kakangu kwa kuileta Hoja hii Bungeni ili ipate kujadiliwa. Ninaomba kuwaheshimu Wabunge wote ambao wameweka sahihi za Hoja hii. Inamaanisha kwamba Wabunge hao walikaa chini na kutafakari kwa kina. Ndiyo maana wakaweka sahihi zao kwenye Hoja hii. Nimesikia mambo mengi ambayo yamesemwa. Nikatulia niyasikie na kuyafahamu. Ninawashukuru wenzangu kwa sababu wamekubali kwamba Prof. Kaimenyi ni mjeuri na hasikii. Ni mtu ambaye anafuata nyayo za mhe Duale za ujeuri na ubabe. Anaishi maisha ya ubabe na kuonyesha kuwa yeye ndiye mambo yote. Watu wa Bonde la Ufa mmeambiwaje na mhe. Duale? Amesema hawezi kuzungumza na mtu yeyote kutoka Bonde la Ufa isipokuwa mhe. Ruto."
}