GET /api/v0.1/hansard/entries/567327/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 567327,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/567327/?format=api",
"text_counter": 352,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Bw. Spika, mheshimiwa anasema hanielewi. Nitamufafanulia jioni tukikutana baada ya futari yake. Kwa sasa, ninaomba aniache niyaseme. Aelewe asielewe, hiyo ni shida yake. Mhe. Spika, ninawomba Wabunge watafakari iwapo wanataka Prof. Kaimenyi aendelee na kazi ama aondoke. Hoja hii inasema tuangalie kama tunaweza kumptatia nafasi nyingine ama la, lakini tumeambiwa kwamba Bunge hili litateua kamati maalum kuangalia jinsi anavyofanya kazi; na kwamba kwa sasa tuendelee mbele ili tuipatie kamati hiyo nafasi ya kuifanya shughuli hiyo. Maoni yangu ni kwamba sidhani kama Prof. Kaimenyi anaweza kuyatekeleza majukumu kwenye kitengo cha elimu. Matatizo aliyonayo ni mengi. Kama angeliweza kuketi chini na kuzungumza na wenzake katika sekta ya elimu – wakiwemo waalimu, Wabunge na hata wazee wa Njuri Ncheke – ili aweze kuridhiana nao, matatizo yake yangekuwa haba. Imebidi alazimishwe ndiyo atoe ng’ombe kwa sababu ya ujeuri na ubambe ninaozungumzia. Yeye ni mpaka asukumwe ndiyo aweze kuitikia mwito."
}