GET /api/v0.1/hansard/entries/567405/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 567405,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/567405/?format=api",
    "text_counter": 430,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Nataka kusema kuwa Prof. Kaimenyi alikuwa mwalimu wangu wa shahada ya udaktari wa meno. Bila yeye, leo hii singesimama hapa kama daktari. Kwa vile alikuwa mwalimu wangu nafikiri namwelewa zaidi. Kuna umuhimu wa sisi kuelewa kuwa kila mtu ana maumbile yake. Inachukua muda kwa mtu ambaye amepata shahada hiyo ya uprofesa kufanya kazi kwa urahisi na watu ambao wamechaguliwa. Tatizo lipo. Tunakubali kuwa tatizo lipo. Mimi kama mwanafunzi wake ningechukua nafasi hii kuwaomba wenzangu kwa kuwanyenyekea, tafadhali nawaomba mwalimu wangu mpatieni nafasi aweze kufanya kazi. Sio rahisi kwa Prof. Kaimenyi kuweza kufanya kazi wakati kila kukicha, Sossion amemlemea kwenye koo. Nilimsikia mhe. Mwandeghu akiongea. Ni kweli kuwa ya mgambo ikilia kuna jambo. Jambo lenyewe ni sasa hivi tuweze kulitatua tuone njia ambayo tutaweza kufanya kazi na Prof. Kaimenyi. Anataka kuwezesha elimu iendelee mbele. Lakini mzigo ambao ameubeba umemkalia kooni na ni mzito. Sisi kama Wabunge wa Bunge hili la Kumi na Moja---"
}