GET /api/v0.1/hansard/entries/567688/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 567688,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/567688/?format=api",
    "text_counter": 133,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Gichigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1909,
        "legal_name": "Samuel Kamunye Gichigi",
        "slug": "samuel-kamunye-gichigi"
    },
    "content": "Asante sana Mhe. Naibu Spika. Ninasimama kuunga mkono huu Mswada ambao mhe Wamalwa ameleta hapa. Wale wanaojua historia yangu ya kuja Bunge hawawezi kuuliza kwa nini ninaunga mkono. Katika uteuzi wa chama cha TNA, chama ambacho nilianza nacho, nilishindwa sana, hata hakukuwa na cha kuongea wala majadiliano. Nilinyang’anywa tikiti kwa sababu chama kilikuwa na wenyewe wakati huo. Wale ambao walitengeneza sheria hii walikuwa na nia nzuri kwa sababu walifikiria Kenya ina demokrasia na haki katika uteuzi wa vyama. Ukweli ni kwamba hatujafika hapo. Isipokuwa wale wachache ambao ni viongozi wa vyama hapa, hakuna mtu atapinga Mswada huu. Labda tu viongozi wachache wa vyama ambao wana hakika kuwa siku ya uteuzi ukifika, wana tikiti mfukoni kwa sababu ndio wanaotia sahihi. Ninawaomba wenzangu kwamba siku ambapo tutasema kwamba ni vyama vichache tu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}