GET /api/v0.1/hansard/entries/567691/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 567691,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/567691/?format=api",
    "text_counter": 136,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Gichigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1909,
        "legal_name": "Samuel Kamunye Gichigi",
        "slug": "samuel-kamunye-gichigi"
    },
    "content": "Nikielekea kumaliza, kuna kitu ambacho ninataka kuuliza. Pesa hizi ambazo zinapatiwa vyama wakati huu na zinachukuliwa na vyama vikubwa zinaenda kusaidia vyama vilivyoko sasa. Kwa nini zisaidie vyama vichache na ziache vyama vingine ambavyo vina viongozi katika Serikali? Sababu ni ipi? Mtu asimame hapa aseme ni kwa nini kama chama changu cha Alliance Party of Kenya (APK), New FORD Kenya ama FORD Kenya visipatiwe na vyama vya TNA na ODM vipatiwe? Sababu ni gani? Mtu atueleze tuelewe kwa sababu sheria iliyoko ni mbaya. Ukiwa Mheshimiwa hapa, hujui ni kipi kitafanyika kesho. Hujui utakuwa wapi, upande wa kulia ama wa kushoto. Chukua kitu tunaita bima kwa kuunga mkono Mswada huu. Ninarudia kwamba siku ile tutakuwa na demokrasia katika vyama ndipo tutakapokubali sheria iliyoko sasa. Kwa wakati huu, tubadilishe sheria na tuwe na haki. Asanteni sana."
}