GET /api/v0.1/hansard/entries/567797/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 567797,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/567797/?format=api",
    "text_counter": 242,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 751,
        "legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
        "slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
    },
    "content": "fulani wakionekana wanashirikiana na upande wa pili, hao ni wasaliti na wanafaa kuadhibiwa. Kwa hivyo, huu Mswada utatusafishia hali ilivyo katika vyama vya kisiasa kwa wakati huu. Pia itatupatia nafasi tuzidi kuongeza vyama. Vyama vikiongezeka humu nchini, demokrasia itaeleweka. Kila mtu atatetea kile chama ambacho anakiona kina msimamo wa kuelekeza mapenzi na uwiano katika jamii zote. Vyama vingi tulivyonavyo leo, tukiwa nje, vinazungumzia uwiano wa jamii. Lakini vikikaa peke yao vinasema: “Ni sisi kama kabila ama nyumba hii.” Hatuwezi kukubaliana na kauli hiyo kwa sababu haielekezi Kenya katika mwelekeo ambao unafaa. Inaelekeza Kenya katika hali ambayo inaleta utata katika jamii. Hizo pesa zikichunguzwa zaidi, tutapata ukweli. Ndiyo mwananchi mlipa ushuru aelewe ni kwa nini vyama vinapewa pesa. Lakini kwa sasa, wananchi ambao pesa zao zinapewa vyama vya kisiasa hawajui zinafanya kazi gani. Hakuna siku utakuta chama kimemwita yule mwananchi kumweleza: “Pesa yako ikikatwa huwa inafanyiwa kazi hii na hii katika chama.” Kwa hivyo, naunga mkono Mswada huu. Mhe. Wamalwa, ahsante sana."
}