GET /api/v0.1/hansard/entries/568299/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 568299,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/568299/?format=api",
    "text_counter": 360,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kamati ya Leba na Maslahi ya Wafanyi kazi iliwaalika washikadau wote ambao wanahusika na pesa za waliostaafu katika kaunti zote 47 katika nchi ya Kenya. Katika mwaliko huo, walikuwemo; Kamati ya Fedha, Biashara na Bajeti ya Seneti, Wizara ya Fedha katika Serikali ya Kenya, Shirika linalohusika na malipo ya uzeeni – RBA, wale wanaohusika na pesa za wafanyikazi katika kaunti zote nchini ambao ni wawili, zikiwemo LAPTRUST na LAPFUND. Vile vile, Kamati yetu ilialika Shirika la Mpito katika nchi ya Kenya (Transition Authority). Pia, tuliweza kualika Tume ambayo inaangalia mishahara ya wafanyikazi katika nchi ya Kenya (The Salaries and Remuneration Commission), the Council of Governors (COG) waliweza kuja na pia tume ya kutekeleza katiba (CIC). Vile vile, kulikuwa na chama kile kinachowatetea wafanyikazi katika nchi ya Kenya ambacho kinahusika na serikali za kaunti. Bw. Spika wa Muda, kati ya hao washikadau wote, tuliweza kuwaita na tukasikiza kwa kina maoni yao. Mengi yalijitokeza, na miongoni mwa yale yaliyojitokeza ni kwamba wafanyikazi wa kaunti zote 47 walikuwa wanasikitika sana kwa ucheleweshaji wa kujumuisha washikadau hawa wawili; LAPTRUST na LAPFUND, ili kuona ya kwamba mashirika haya mawili yanayoweka pesa za wafanyikazi ambao wanafanya kazi katika kaunti zote, ambazo ni pesa nyingi, wao wako na wasiwasi na hawawezi kujua kama pesa zao zitawekwa vizuri, hali ya kwamba ikiwa watastaafu, basi pesa hizo hazitakuwa na ufujaji wa aina yoyote. Tuliweza pia kufahamu kwamba kuna kaunti zingine katika nchi ya Kenya ambazo zinachukua pesa hizi za wafanyikazi ambao wamestaafu katika kaunti na wale walioko hivi sasa na watastaafu. Wakishazitoa pesa hizi kwa mishahara yao, hawazipeleki kwa hawa washika dau wawili. Inafaa wapeleke kwa LAPTRUST ama kwa LAPFUND lakini hao huziweka. Kwa hivyo, kumekuwa na wasiwasi kwamba, je, watazipata wakati watakapostaafu? Hilo ndilo swali kubwa ambalo tuko nalo. Katika Kamati vile vile, tuliweza kusikia tetesi mbali mbali. Lakini kwa sababu sisi kama Kamati tumeangalia na tumeona kwamba ingefaa kama tungewaita hawa washikadau wote pamoja kwenye kongomano kubwa. Tukiwaweka pamoja, tutafanya vile makadinali wanafanya wakati wanapomchagua Baba Mtakatifu. Tutawaweka pamoja mpaka tuone moshi mweupe. Kwa hivyo, sisi kama Kamati ya Labour and Social Welfare tutakuwa na kongamano. Tutawaita washikadau wote ambao tumewataja hapo awali. Miongoni mwao ni Council of Governors (CoG) na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya wafanyakazi. Kila mtu atapewa nafasi ya kuzungumza ili tuseme yale tutakayosema. Ikiwa kutakuwa na ratiba na memoranda zitakazokuwa zimeandikwa, tutazichukuwa. Endapo watakuwa na mambo ya kusema, tutayasikiliza. Hiyo inamaanisha kuwa kutakuwa na mabadiliko mengi katika Mswada huu. Bw. Spika wa Muda, kwa sababu tunataka kila mtu atosheke, kila mtu atapewa nafasi ya kutoa maoni yao. Kamati hiyo itakayojumuisha sisi hapa kama Seneti na Bunge la Taifa itakaa na kuchanganua maoni yote ili tupate mwelekeo. Hiyo itakuwa baada ya kongamano kubwa tutakalokuwa nalo kuanzia tarehe tatu hadi tarehe 26 mwezi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}