GET /api/v0.1/hansard/entries/568301/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 568301,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/568301/?format=api",
    "text_counter": 362,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "huu wa saba. Tutawaalika washikadau wote na Seneti ili tuweze kujadiliana. Ikiwa kutakuwa na maoni tofauti tofauti, tutayachanganua wakati huo. Baadaye, tutarudi hapa na kuangalia mageuzi yatayopendekezwa katika Mswada huu. Huenda yakawa mengi na yatatusaidia. Tutayajumuisha maoni hayo katika Mswada huu kabla ya kuuleta hapa tena. Seneti itaamua kutengeneza mabadiliko ili kuendelea na Mswada huu baada ya kuchukuwa maoni ya watu wote na kuyaweka pamoja ili kujua mwelekeo utakuwa upi. Hatari moja katika Mswada huu ni kwamba viongozi wengi wa siasa wanachaguliwa na wananchi kwa muda. Hatuwezi kuacha pesa hizo nyingi katika mikono iliyo na muda wa kutelekeza majukumu ikilinganishwa na siasa tuliyonayo. Huenda ukawepo leo na kukosa kuwepo kesho. Lazima pesa za wafanyikazi ziwekwe katika benki na kuwa na mkataba kati ya washikadau na Serikali ambao hauwezi kubadilishwa. Tunafaa kuhakikisha kuwa pesa za wafanyikazi ziko mahali pema ambapo hakuna mtu anaweza kuzivuja. Hii ni mipangilio ambayo sisi kama Kamati ya Labourand Social Welfare tunayo. Tunanuia kuwa wakati tutakapopeleka barua sehemu mbalimbali kuwaalika washikadau, wote watakuja ili tujadiliane. Mwisho, Bw. Spika wa Muda, tumeona ya kwamba mwelekeo unahitajika katika pesa ambazo sasa hivi hazipelekwi katika Local Authorities Pension Trust (LAPTRUST) ama Local Authorities Pension Fund (LAPFUND) . Nia ya Kamati hii kutengeneza mwamvuli ambao utajumuisha hawa washikadau wawili, LAPTRUST na LAPFUND, na kuwaweka pamoja. Watatakikana kutengeza mwamvuli wa sheria ambapo kila mfanyakazi atajua kuwa pesa zake ziko mahali pema na salama. Hiyo ndio nia ya Kamati. Ni kwa sababu hii ninaunga mkono Mswada huu. Nampongeza ndugu yangu; Kiongozi wa Walio Wengi katika Seneti, kwa kuleta Mswada huu. Asante sana, Bw. Spika wa Muda."
}