GET /api/v0.1/hansard/entries/568936/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 568936,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/568936/?format=api",
"text_counter": 207,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Mhe. Naibu Spika ninaomba nitoe mwongozo wangu. Wewe hukusoma huko lakini ulikuwa unafundisha. Hivi sasa tunakubali huyu mama, Anne Gitau apatiwe kazi hii. Ninaomba tuulizane maswala kadha wa kadha. Ningependa tuangalie Katiba inasema nini. Katiba inaongea kuhusu usawa wa nchi. Kwa nini kila wakati majina yakiletwa hapa yanaletwa ya maeneo mawili tu? Majina yanatoka Bonde la Ufa ama eneo la Kati. Nikisema hivi si eti ninamchukia mtu. Mimi simchukii mtu. Bi. Gitau amehitimu na ana kila kitu lakini ningependa kusema kwamba wako Wakenya wengine. Mimi sina shida na huyu shangazi. Ninamheshimu, amehitimu, ana sifa, ana elimu na ameenda college, Egerton. Kwa hivyo, sikatai lakini kama tunataka usawa katika nchi hii, lazima tujue kwamba majina mengine yako pia. Wataita, Waluhya, Wakamba, Wasomali, Wadorobo na Waogiek wako. Hawa watu wameachwa wapi? Kila wakati majina yanayoletwa hapa ni ya makabila mawili. Kwa nini? Hata Mwenyekiti wa Tume hii anatoka Bonde la Ufa."
}