GET /api/v0.1/hansard/entries/570734/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 570734,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/570734/?format=api",
    "text_counter": 164,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, asante kwa kunipa nafasi hii niunge mkono Mswada huu. Pia ninataka kumpongeza Seneta kijana shupavu, wakili ambaye ni Seneta wa Nandi, Sen. Sang. Ni jambo la muhimu kwake kuleta Mswada huu. Kwa mara ya kwanza tangu tupate Uhuru, tunaona mwelekeo hasa katika Serikali zetu za ugatuzi. Hii imekuwa changamoto hasa tukiangalia wakati huu ambapo tumepoteza mtu shupavu nchini. Huyu ni mtu ambaye tangu Kenya ipate Uhuru, amekuwa akichekesha watu, amekuwa akichekesha taifa nzima katika kipindi kinachoitwa Vitimbi . Huyu ni Mzee Ojwang. Hivi sasa sisi sote tunaomboleza kama taifa kwa kumpoteza Mzee Ojwang. Yeye alikuwa anajulikana hata na watoto wachanga. Sisi wenyewe tumekuwa tukimtazama huyu mzee katika televisheni akichekesha wananchi. Hivi leo ni jambo la aibu kwamba mzee kama huyu amekufa kama mtu ambaye hakuwa anajivunia kuwa Mkenya. Hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kusema kwamba Serikali ilimjengea nyumba, kumfanyia jambo fulani ama kumtambua tu kwa sababu ya vitimbi vyake kwa miaka 30. Tunasema kwamba hili ni jambo la aibu. Inatakikana wakati mtu akifanya kitu chema kama vichekesho ama usaidizi kwa Wakenya, ni lazima taifa letu liweze kumtambua. Hivi sasa tunasema kwamba Mwenyezi Mungu amuweke Mzee Ojwang mahali pema peponi. Wananchi wakati huu ni lazima waelewe kwamba sisi kama Seneti tumeona kwamba Mswada huu ni muhimu kwa wale ambao wametoa maisha yao kusaidia nchi au Serikali. Tunajua kwamba jambo kama hili, kumekuwa na mapendeleo, kujuana na njia tofauti tofauti ama mbinu ambazo watu wanatumia kupata shahada kama hizi zinazotolewa na Serikali kuu. Kuna EGH, OBS na kadhalika. Watu wamekuwa wakizipeleka kwa jinzia ya urafiki na kwa kujulikana ili kutambuliwa na Serikali kuu. Sasa wakati umefika wa kaunti kupewa uwezo wa kutambua watu ambao wamefanya vitu ama waliotenda vitendo ambavyo viliweza kusaidia kaunti ambazo walitoka. Tunajua wahenga walisema ya kwamba mwacha mila ni mtumwa. Ikiwa wewe umeishi katika ulimwengu na umewacha asili yako, unafanya vitu vya kizungu, umeendelea ama umesoma na hutaki asilia yako, basi wewe ni mtumwa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}