GET /api/v0.1/hansard/entries/570736/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 570736,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/570736/?format=api",
"text_counter": 166,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kipengele 3 cha Mswada ambao Sen. Sang ameuleta, kinaeleza maana kwa kina cha Mswada huu. Kipengele 3(a) kinaeleza kuhusu watu ambao wamejitolea maisha yao, kuweza kuinua hali ya maisha ya watu ambao watakuja baada yao wakishaenda mbele za haki. Kipengele 3(b), kinazungumzia kuhusu kutambulika kwa watu ambao wameweza kuweka historia, kulinda na kuelimisha asili ama mienendo ya watu ambao wanaishi katika eneo au kaunti ambazo wametoka. Hii inamaanisha ya kwamba kunayo mipangilio kabambe ambayo mtu hawezi kuchaguliwa ikiwa hatakuwa amewajibika katika sheria hiyo ya Kipengele 3. Tunajua watu ambao wameenda mbele za haki, hapo zamani, ambao walikufa, hivi sasa tunawaita marehemu. Kama alivyo sema ndugu yangu Sen. Sang, tuko na watu shupafu waliopigania Uhuru katika Kaunti ya Kilifi. Uhuru haukupiganiwa na Mau Mau pekee yake. Ulipiganiwa na Wakenya katika pande zote za Kenya. Pande zetu za Pwani, tulikuwa na watu kama Mekatilili wa Menza, Mepoho na pia tunatambua marehemu Emmanuel Karisa Maitha. Kama marehemu Karisa angekuwa anaishi, watu wa Pwani hatungekuwa tunababaika leo. Tungekuwa na msimamo kabambe kuhusu kura zinazokuja mwaka 2017. Lakini yeye ni marehemu na sisi tutaendelea kufuata ndoto yake. Tunasema kuwa, hao watu waliweza kusaidia jamii zao lakini kuna mabibi wa waume shupavu. Tuko na mama bibi ya marehemu Ronald Gideon Ngala, aliyekua shupavu wa kisiasa katika mkoa wa Pwani. Mama huyo bado anaishi. Kuna wazee wengine wa Kaya ambao huwa wanaelezea mwelekeo. Wengine walifariki na wangine bado wako. Bw. Spika wa Muda, katika Mswada huu kuna vipengele ambayo vinasema serikali za kaunti zitatakikana kujenga nyumba au jumba ambako kutawekwa vigango ambavyo vitaweza kueleza historia na asili ya watu kuanzia vizazi vilivyokua hapo awali hadi sasa. Hivi juzi, maofisa kutoka Kaunti ya Nairobi waliweza kualikwa Marekani. Walienda kuchukua vigango ambavyo vingi vyao vilikua vya Kaunti ya Kilifi. Baada ya kuvichukua vigango hivyo, kutoka Marekani, walikuja nazo hadi Nairobi lakini hivi sasa havijafika Kilifi. Hata wakivileta huko Kilifi, hatujui tutaviweka mahali gani. Ndio sababu katika huu Mswada tunasema ya kwamba vigango hivyo ama “artifacts ” kwa lugha ya Kiingereza lazima ziwekwe mahali---"
}