GET /api/v0.1/hansard/entries/570742/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 570742,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/570742/?format=api",
"text_counter": 172,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kutengezwa zamani na kuchukuliwa ili ile sura ya Koitalel arap Samoei isipotee. Katika vile vigango walivyovitengeza, wajukuu, vitukuu na kitukuu wa jemedari Koitalel, kama Sen. Sang na wale waliokwenda mbele yake, wanaweza kufahamu sura zao zilikua za aina gani. Vigango ni vitu ambavyo hatuwezi kuvisahau katika historia yetu. Sisi tunasema ya kwamba katika Mswada huu, kuna kamati ambayo itaongozwa na naibu wa gavana. Katika hiyo kamati watapewa mamlaka ambayo mtu atakayechaguliwa lazima aingie katika ile historia. Wananchi pia watapewa nafasi ya kualikwa ili watu ambao wamechaguliwa waingie katika huu Mswada; wananchi wataweza kuandika barua na kuongea kuhusu yule mtu ambaye atakuwa amechaguliwa kuingia katika historia hii. Hiyo inamaanisha ya kwamba, hakutakuwa na mapendeleo. Haitakuwa kama vile ukitaka hadhi ya serikali ama Elder of Golden Heart ( EGH), itakua umefanya kitu bora katika Serikali kuu. Hivi sasa, ni lazima wananchi wa kaunti wahusishwe na waamini ya kwamba huyu mtu ni ukweli alileta faida fulani katika historia ya kaunti. Katika Mswada huu, mtu akipatikana amesema uongo atapatikana na hatia na ataadhibiwa. Anaweza kutozwa faini ya Kshs1milioni, kufungwa kwa miaka miwili ama apigwe faini na pia kupelekwa ndani. Kutakua na sheria mufti ambazo zitahakikisha ya kwamba hakutakua na upendeleo na watu kusema uongo. Ukipatikana umefanya kitendo kama hicho kutakuwa na sheria za kukuadhibu. Tunasema sisi tunataka Mswada kama huu uwepo. Naunga mkono ndugu yangu kwa kuleta Mswada huu wakati ambao tunahitaji zaidi ili tuweze kutambua wale wazee wetu waliotufanyia mema na ambao walituweka mahali tulipo. Itakua ni aibu ikiwa wale wazee walitusomesha kwa pombe ya mnazi. Hivi sasa watu wanashikwa wakitengeneza na kunywa pombe ilhali sio haramu. Pombe hiyo haiwezi kudhuru au kuleta hasara yoyote kwa mwananchi. Pombe hiyo ni kama barafu ya mwili wa binadamu. Kwa hivyo, namuunga mkono ndugu yangu, Sen. Sang, kwa kuleta Mswada huu. Nataka kumhakikishia kwamba Kamati yetu ya Leba na Maslahi ya Jamii itaangalia Mswada huu vizuri na tutaleta marekebisho hapa Seneti. Nina hakika kwamba Maseneta shupavu walio hapa, watawasiliana na kuupitisha. Asante sana Bw. Spika wa Muda. Ninaunga mkono Mswada huu."
}