GET /api/v0.1/hansard/entries/571547/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 571547,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/571547/?format=api",
    "text_counter": 144,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika. Nachukua nafasi hii kukupongeza kwa uongozi na uwazi katika uamuzi wako ambao sisi tunaweza kusema pengine ulitekelezwa wakati wa Mfalme Solomoni. Tunausifu uongozi huo kama Maseneta. Kulingana na Katiba yetu ya Kenya, Kipengele cha Kwanza, uongozi wa nchi hii ni jukumu la Bunge. Jukumu hilo linatekelezwa na viongozi waliochaguliwa. Sio mara ya kwanza au ya pili kwetu Maseneta kuona kwamba Rais amechukua mwelekeo usiolingana na Katiba.Tukizingatia zaidi ile Miswada ambayo imetoka katika Bunge la Kitaifa ikipuuza Bunge la Seneti. Hili ni jambo hatari na jukumu hili liko katika mikono yake Rais wa Nchi hii. Yeye kama Rais ana uwezo wa kukataa kutia sahihi na kukuuliza hisia zako kulingana na Mswada unaopelekwa kwake kutiwa sahihi, haswa ikiwa tumejadiliana hapa Seneti na uamuzi wetu ni wa aina gani. Bw. Spika, ikiwa Rais atapuuza msimamo au mkondo kama huo ambao unalingana na Katiba, hii ina maana kwamba Rais wa nchi hii anavunja sheria ndani ya Katiba. Ikiwa kitendo kama hiki kitaendelea, sisi kama Seneti tuna mamlaka, kulingana na Kipengele cha Katiba Nambari 96 kinachosema kwamba Bunge la Seneti lina uwezo wa kumuachisha kazi Rais. Maoni yangu ni kama yale ya ndugu yangu, Seneta wa Kakamega ambaye amesema, kwamba kulikuwa na upuuzi na Bunge la Seneti halikuhusishwa katika uamuzi kuhusu uteuzi wa Gavana wa Benki Kuu ya Kenya. Hata kama ni mzuri wa aina gani, kwa maoni yangu, ikiwa uteuzi huo ulifanywa bila kuambatana na sheria, ni bora waambiwe wakae kando ili Bunge la Seneti lijadiliane na kukubaliana ili sisi nasi tupeleke maoni yetu kwa Rais. La sivyo, ni vizuri Seneta wa Kakamega atengeneze Hoja itakayokuja hapa Seneti, tujadiliane na kuweke historia katika Bunge hili. Asante sana, Bw. Spika."
}