GET /api/v0.1/hansard/entries/572224/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 572224,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/572224/?format=api",
    "text_counter": 189,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Bule",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1029,
        "legal_name": "Ali Abdi Bule",
        "slug": "ali-abdi-bule"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, nataka niwaeleze na niwaelimishe Maseneta ambao hawaelewi. Mimi kama Sen. Bule, nimechaguliwa kwa tiketi ya FPK, ambayo ilikuwa kwa chama cha CORD, na muungano si chama. Ni muungano wa kufanya kazi pamoja. Mimi baada ya kuchaguliwa, tuliamua kama viongozi wa FPK kufanya kazi pamoja kwa sababu yule ambaye alimwoa mama ndiye baba. Kwa hivyo, tuliamua kufanya kazi na Chama cha Jubilee, lakini wameshindwa kuwa baba. Sisi kama wana wa FPK tumeamua kufanya kazi na chama ambacho kitaweza kuwa baba hata kesho."
}