GET /api/v0.1/hansard/entries/572400/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 572400,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/572400/?format=api",
"text_counter": 365,
"type": "speech",
"speaker_name": "July 23rd, 2015 SENATE DEBATES 47 Sen. Chiaba",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii niunge mkono Hoja hii iliyoletwa na Sen. Orengo. Imekuja wakati unaostahili. Anayekuja hapa si Rais wa kawaida; ni Rais wa taifa lenye ushawishi mwingi katika ulimwengu, Taifa la Amerika. Tukijaribu kufananisha Rais wa Amerika na rais yeyote huko Uropa, Asia au Afrika, tunajidanganya. Rais wa Amerika ni wa kipekee. Ni mtu ambaye anatawala dunia nzima. Anaongoza dunia nzima kuleta amani na biashara. Tunatarajia mengi kutoka kwa mtoto wetu. Zaidi ya hayo, huyu anayekuja si tu Rais wa Taifa la Amerika bali wazazi wake wanatoka hapa Kenya. Tunatarajia mema atakayetuletea, akikumbuka kwamba wazazi wake wanatoka sehemu hii ya Afrika. Ninatambua juhudi zake za kuleta mambo mengi ili kusaidia mataifa ya Kiafrika. Zaidi ni kwamba Taifa la Amerika ni taifa linalozingatia vipengee vya Katiba. Kama hawangetegemea hiyo, Rais Obama hangekuwa Rais wa taifa hilo la Marekani. Yeye ni Rais wa 44 wa Marekani. Ni Rais ambaye wazazi wake wametoka Kenya. Marais wengine 43 wana asili ya Uingereza na Ireland Kusini. Wengine ni Wakotoliki, na wengine ni Protestanti lakini yeye wazazi wake ni Waislamu. Hilo ni dhihirisho kwamba Maerikani ni taifa kubwa ulimwenguni. Ningependa pia kumjibu Kiongozi wa Wachache katika Seneti aliyesema kwamba Jubilee haijawaangalia watu wa Kaunti ya Lamu. Ninamkumbusha ya kwamba Katibu wa Kudumu katika Wizara ya Ardhi na Balozi wa Kuwait wanatoka Lamu. Pia, nachukua fursa hii kumpongeza Waziri wa Maswala ya Kigeni na Biashara ambaye kwa juhudi anayofanya kuleta uhusiano bora katika mataifa yote ya ulimwengu. Kwa hayo machache, naunga mkono."
}