GET /api/v0.1/hansard/entries/572416/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 572416,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/572416/?format=api",
    "text_counter": 381,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Ukiona vyaelea, jua vimeundwa. Marekani sio nchi ambayo tunaweza kushindana nayo. Kwetu sisi ni nchi ya kuiga. Kwa hivyo, tutafanya kila juhudi tuwaige kwa sababu kila safari ndefu huanza na hatua chache. Nasema hivyo kwa sababu tutabaguana na kupakana matope, lakini mgeni akija ni lazima tuwe na nidhamu kama Wakenya. Bi. Spika wa Muda, katika swala la usalama, Waswahili husema kwamba ukiona mti unapurwa, jua ya kwamba una matunda matamu. Juzi tumekuwa na wageni, wake wa marais kutoka nchi maridhawa. Huo si ugeni mdogo bali ni juhudi za nchi yetu. Marekani pia haikuanza hivi hivi. Lazima Rais Obama aliungwa mkono na watu wake kwa sababu nguvu za maji ni mawe. Sisi hapa hatuthamini watu wetu wenyewe. Rais Uhuru na Makamu wake ni viongozi wetu lakini je, sisi tunawaunga mkono? Kwa nini tusiwaunge mkono ili tupate ile sifa? Tunaona tu lazima wawe kama Rais Obama. Hatuwezi kushindana naMarekani. Naomba hata sisi tuiunge Serikali mkono na tuige Marekani.Hata upande wa nidhamu, kila kitu lazima kitachukua muda. Bi. Spika wa Muda, ninampa kongole Sen. Orengo kwa Hoja hii kwa sababu mgeni lazima akaribishwe na sisi tunamkaribisha Rais Obama nyumbani. Tunatamani hata sisi tungempa omena ale ili apate nguvu kwa sababu watu wake wana nguvu. Ninaunga mkono Hoja hii."
}