GET /api/v0.1/hansard/entries/573102/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 573102,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/573102/?format=api",
    "text_counter": 278,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Juma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13130,
        "legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
        "slug": "zuleikha-juma-hassan"
    },
    "content": "Ahsante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii kuzungumza kama mwakilishi wa vijana katika nchi hii ya Kenya hapa katika hili Bunge la Kitaifa. Nilifurahi sana kwa sababu ya Hotuba ya Rais Obama. Nilikuwa huko Kasarani. Sababu ya kufurahi ni kuwa mazungumzo mengi yalikuwa juu ya masuala ya vijana. Pia, nilifurahi kwa sababu waliokuwa wengi zaidi katika kongamano hilo ni vijana. Pia, nilifurahi tena zaidi kuwaona vijana kutoka kaunti yangu - ambayo inatajwa kuwa nyuma katika masuala ya maendeleo. Wengi wao zaidi walikuwa ni wasichana."
}