GET /api/v0.1/hansard/entries/573105/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 573105,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/573105/?format=api",
"text_counter": 281,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Juma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13130,
"legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
"slug": "zuleikha-juma-hassan"
},
"content": "Pia nafurahi kuwa kiongozi wetu wa chama chetu cha Orange Democratic Movement (ODM), Mheshimiwa Raila Amolo Odinga, anaunga mkono masuala ya vijana. Chama chetu cha ODM ndicho cha kwanza kilichoanzisha Youth League ama Bawa la Vijana katika vyama vya kisiasa humu nchini. Ndicho chama cha kwanza kuweza kufanya jambo kama hilo. Hapa Kenya tunayo suluhu kwa shida za vijana wetu. Suluhu moja ambayo sisi kama Wabunge tunaweza kusaidia ni kuhakikisha kuwa tunabadilisha sheria za National Youth Council (NYC). Mimi nimeshaanza kufanya hivyo na Mungu akipenda, itakuja hapa Bungeni hivi karibuni. Mhe. Koffi Annan alipokuja Kenya baada ya vita vya mwaka wa 2007/2008, alihimiza sana kuwe na baraza la vijana au National Youth Council . Umuhimu wa baraza hilo ni kuwapatia vijana nafasi ya kufanya kazi katika vijiji vyao ama katika maeneo yao. Kama vile Rais Obama alivyosema, yeye alianza na community work huko Chicago ndio ikamfundisha masuala ya uongozi bora. Kwa hivyo, hilo baraza la vijana litawapatia nafasi Wakenya kutoka kila sehemu hapa nchini. Vijana wa kila kabila hapa nchini watapata fursa ya kujifundisha uongozi bora. Kitu kingine ambacho baraza la vijana linaweza kusaidia ni kuwapa vijana nafasi muafaka ya kuweza kuzungumzia masuala ambayo yanawasumbua kama vile ugaidi. Vile vile, ningependa kuiomba Serikali ilipatie baraza hilo la vijana pesa inavyostahili kwa sababu tayari limeundwa kisheria. Baraza hilo litawafundisha vijana njia za kupigana na ufisadi. Pia, litawapatia vijana nafasi ya kuota ndoto zao. Vijana ni lazima wachukue uongozi. Naomba tuwapatie nafasi za kuwafundisha uongozi mzuri kupitia kwa baraza la vijana - the National Youth Council. Ahsante."
}